Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM uko tayari kusaidia waathirika wa tetemeko Iran-Iraq

UM uko tayari kusaidia waathirika wa tetemeko Iran-Iraq

Pakua

Umoja wa Mataifa uko tayari kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Jumapili jioni mpakani mwa Iran na Iraq na kusababisha vifo na uharibifu mkubwa endapo utahitajika kufanya hivyo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake, akiongeza kuwa ameshtushwa na athari zake, huku akitoa pole kwa familia za waathirika na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi.

Mashirika mbalimbali ya kitaifa na kimataifa likiwemo la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA na timu ya uokozi ya kujitolea ya chama cha msalaba mwekundu Iran na Iraq yanahaha kuendelea kusaka manusura na kutoa huduma ya kwanza kwa majeruhi.

Kwa mujibu wa mashirika hayo watu 328 wamepoteza maisha na wengine 3950 kujeruhiwa huku idadi hiyo ikitarajiwa kuongezeka.

Chama cha msalaba mwekundu Iran kinasema athari kubwa iko upande wa Iran kwa vifo na majeruhi. Iraq hadi sasa watu waliotajwa kupoteza maisha ni 9 na majeruhihi ni 425.

Miji iliyoathirika ni Qasre-Shirin, gilane-Garb, Kermanshah, sare-PuleZahab, salase-Babajani, Dalahoo na Islamabad.

Photo Credit
UN Photo/John Isaac