Tunahitaji fedha za dharura kusaidia wakimbizi wa Iraq: UNHCR
Idadi ya wanaofurushwa makwao ikiongezeka Magharibi mwa Mosul nchini Iraq, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linafungua kambi mpya sambamba na wito wa usaidizi kwa wafadhili kuongeza fedha kwa ajili ya ulinzi na malazi kwa wanaofurushwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR, watu 255,000 wamefurushwa kutoka Mosul na maeneo ya karibu tangu mwezi Oktoba mwaka jana, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 100,000 tangu kampeni ya kijeshi iliponza Magharibi mwa mji huo mnamo Januari 19.