Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunawasaka waliotekwa nyara DRC-Dujarric

Tunawasaka waliotekwa nyara DRC-Dujarric

Pakua

Umoja wa Mataifa umesema unaendelea na msako dhidi ya wataalamu wa kimataifa wawili na wafanyakazi watatu raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC ambao walitekwa nyara na watu wasiojulikana jimboni Kasai nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja huo Stéphane Dujarric amesema malalamiko ya serikali ya DRC kuhusu kutoarifiwa kuhusu uwepo wa wafanyakazi hao yatajibiwa na maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini humo na kuongeza kuwa kwa sasa mwelekeo ni kuendelea kuwasaka watu hao walioko kusikojulikana.

Akijibu swali kuhusu hisia za ndugu na jamaa wa wafanyakazi walioshikiliwa Dujarric amesema.

(Sauti Dujarric)

‘‘Naelewa kwa hakika, shauku za familia ya watu waliohusika, na watu walio karibu nao. Napenda kukuhakikishia kwamba Umoja wa Mataifa unafanya kila uwezalo, umepeleka vifaa eneo hilo na tunaendelea kuwatafuta.’’

Duru zinasema kuwa wataalamu wa kimataifa waliotekwa nyara mmoja ni raia wa Marekani na mwingine wa Sweden.

Photo Credit
Msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja huo Stéphane Dujarric akihutubia waandishi habari.(Picha:UM/Mark Garten)