Zaidi ya watu milioni 7 wanakumbwa na baa la njaa bonde la ziwa Chad:UM
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo liko nchini Chad ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya nchi nne kuangazia changamoto zinaoendelea za kibinadamu katika eneo la bonde la ziwa Chad na kuongeza uelewa wa kimataifa kwa hatma ya watu wapatao milioni 11.
Ujumbe wa baraza hilo ukiwa katika mji mkuu N'Djamena umekutana na waziri mkuu Albert Pahimi Padacké na pia kutembelea kikosi cha pamoja cha askari kutoka nchi nne zilizoathirika kwenye kanda hiyo ikiwemo Cameroon, Chad, Niger na Nigeria, pamoja Benin wanakokabiliana na mapambano dhidi ya Boko Haram.