Uhai wa wanyamapori ni uhai wetu- UNEP

Uhai wa wanyamapori ni uhai wetu- UNEP

Pakua

Tarehe tatu mwezi Machi ya kila mwaka ni siku ya wanayamapori duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kusikiliza sauti za vijana ambao wana fursa ya kuhakikisha urithi wa wanyamapori kwa vizazi vijavyo.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP, kuwaenzi wanyamapori na maliasili ambalo ni jumuku la serikali na sekta binafsi na hata raia linahitaji hatua madhubuti na hivyo katika ujumbe kupitia tovuti hususani Twitter, shirika hilo limehamasisha dunia kulinda viumbe hai na maliasili kwa kusema “ Fanya jambo moja leo”

Photo Credit
Tempo wanaopatikana barani Africa. Picha: World Bank/Curt Carnemark