Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ITC kuinua wanawake kiuchumi Rwanda

ITC kuinua wanawake kiuchumi Rwanda

Pakua

Kituo cha kimataifa cha biashara ITC ambayo ni taasisi tanzu ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD na wadau, hii leo wametangaza ushirikiano mpya ili kusaidia wauzaji wa kahawa nje ya nchi, wasindikaji, na wakulima wa zao la buni nchini Rwanda.

Ushirikiano huo unalenga uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ambapo uboreshaji uwezo wa wa usindikaji wa kahawa nje ya nchi , kuongeza ubora wa zao hilo, kuongezeka kwa bei na kupunguza uchafuzi wa mazingira na matumizi mema ya maji vitazingatiwa.

Taarifa ya ITC inasema kuwa wadau hao watatoa mafunzo kwenye kitengo cha usindikaji cha uchumi wa kilimo ili kuhakikisha viongozi wa wakulima wana uwezo wa kutathmini mahitaji ya wakulima na kuwa na zana za kushauri na kuwaongoza na pia kuwa na mawasiliano bora.

Kampuni shiriki katika mradi huo ni Sucafina pamoja na Jacobs Douwe Egberts.

Photo Credit
UN Photo/Martine Perret