Ushirikiano wa nchi za Kusini-kusini ni muhimu kwa ajenda ya 2030: Ban

Ushirikiano wa nchi za Kusini-kusini ni muhimu kwa ajenda ya 2030: Ban

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema kuwa ushirikiano zaidi kwa nchi za kusini-Kusini ni muhimu kwa mafanikio ya kiuchumi duniani na kuendeleza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.

Katika ujumbe wake kwa njia ya video kwenye maonyesho ya kimataifa ya nchi za Kusini-Kusini kwa ajili ya maendeleo huko mjini Dubai Emarati, Ban amekaribisha uamuzi wa tukio hilo la kuzingatia jukumu kuu la nchi za Kusini na ushirikiano kwa pande zote wa kufuatilia teknolojia katika kuboresha mazingira, uvumbuzi wa viwanda, na kuboresha kimataifa afya nauhakika wa chakula. Ameongezea kuwa changamoto hizi zinaathiri ufikiaji wa SDGs na amewasihi washiriki wote, kujenga na kuendeleza mikakati endelevu kwa manufaa ya wote.

Naye mkurugenzi ya Ofisi hiyo ya ushirikiano wa nchi za Kusini-Kusini Jorge Chediek akihojiwa na idhaa hii amesema huu ni mkutano unaofanyika kila mwaka kuangazia yapi mapya katika kuongeza ushirikiano zaidi kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu. Amesema nchi za kiarabu zimepiga hatua

(Sauti ya Jorge Chediek)

"Ijapokuwa wamepiga hatua kwa kuendeleza utoaji wa vifaa vya petrol, jambo la kujivunia wameweza kubadilisha nchi iliyokuwa jangwa na mji wa Dubai kuleta maendeleo kama vile kwa utalii, kiuchumi, na kifedha kwa manufaa ya jamii na wengine wote."

Photo Credit
Jorge Chediek.(Picha:UN Radio)