Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

Mitindo ya mavazi huhifadhi mazingira: Akinyi

Umewahi kufikiria kuwa mitindo ya mavazi yaweza kutumika kulinda na kuhifadhi mazingira?

Asilani hilo lawezekana. Katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa idhaa hii, mwanamitindo mashuhuri kutoka Kenya, Akinyi Odongo ambaye ni mmoja wa wanaufaikia wa mradi wa Shetrade wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD wa kuwawezesha wanawake kuingia katika biashara ya kimataifa, anaekleza uhusiano kati ya mazingira na mitindo.

(SAUTI AKINYI)

Mwanamitindo huyu pia anatumia fursa alizonazo katika kuwainua wanawake wengine.

( SAUTI AKINYI)

Watoto wakumbwa na madhila ya vifo wakisaka maisha bora

Mapema juma hili jamii ya kimataifa imefahamishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto kuwa maisha ya maelfu ya watoto wa Amerika ya Kati yako shakani. Wengi hutumbukia katika hatari hizo kwa kusaka maisha bora ughaibuni.

Katika makala ifuatayo Rosemary Musumba anaeleza mazingira hatarishi yanayowakabili watoto hao ikiwamo vifo na madhara mengiee ya kimwili.

UN Photo/Pasqual Gorriz

Kamanda mpya wa UNFIL afanya mkutano wake wa kwanza

Kamanda na Mkuu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, Meja Generali Michael Beary leo ameongoza mkutano wake wa kwanza kwa pande zote tatu na viongozi waandamizi.

kutoka Jeshi la Lebanon na ofisi ya ulinzi ya Israeli katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Ras Al Naqoura. Majadiliano hayo yamehusisha masuala yanayohusiana na utekelezaji wa mamlaka ya UNIFIL chini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa azimio nambari 1701 (2006) kuhusu ukiukwaji huko Blue Line kama vile suala la uondoaji wa majeshi ya Israeli kutoka kaskazini mwa Ghajar.

UN Photo/Eskinder Debebe)

Ban azungumza na Rais wa Italia Sergio Mattarella

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, leo Alhamisi amezungumza na Rais wa Italia Bwana. Sergio Mattarella. Katibu Mkuu ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais huyo na watu wote wa Italia kufuatia vifo na uharibifu mkubwa uliosababishwa na tetemeko la ardhi la asubuhi ya Agost 24 ambapo mamia ya watu wamepoteza maisha.

Pia amepongeza juhudi kubwa na za haraka za uokozi zinazofanywa na serikali ya Italia , kuwanusuru na kuwasaidia walioathirika na tetemeko hilo.

Ban apongeza serikali ya Colombia na kundi la FARC-EP kwa muafaka

Miaka Minne iliopita serikali ya Colombia na kikundi cha waasi FARC-EP walifikia muafaka wa kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda mrefu. Hatimaye hitimisho la mazungumzo ya kutafuta amani limefiakia ukingoni na wanatarajia  kuwatangazia  wananchi matokeo ya mstakabali wa taifa lao.

Katiku Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban-ki- moon kwa furaha kubwa amempogeza raisi wa Colombia Bw. Juan Manuel Santos, kiongozi wa upinzani Timoleon Jimenez na timu nzima ya washauri kutoka Havana kwa jitihada zao za kuhakikisha mazungumzo ya kutafuta amani nchini Colombia yanazaa matunda.

UN Photo/JO (file)

Ban aridhishwa na ripoti kuhusu hayati dag-hammarskjold

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon, anfurahia kutangazwa upya kwa ripoti yake inayoufuata kile alichokitoa mwaka wa 2015 katika jopo huru la wataaalamu liloteuliwa naye kufuatia kauli za Baraza kuu. Jopo hilo liliundwa kushughulika na habari mapya iliyotokea kuhusu kifo cha ghalfla cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hayati Dag-Hammarskjold na wale aliosafiri nao.

UN Photo.

Wataalamu wa haki na biashara wa UM kuzuru Mexico

Kikundi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaojishughulisha na mambo ya biashara na haki za binadamu watatembelea nchini Mexico kuanzia Agosti 29 had Septemba 7 mwaka huu.

Ziara hiyo ni kwa ajili ya kuchunguza jitihada za serikali na makampuni tofauti ya biashara ili kuzuia na kushughulikia athari mbaya za haki za binadamu kwenye biashara. Mexico ni nchi kubwa na ya pili katika Amerika ya kusini kuwa na viwanda vikubwa katika sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na umeme, magari na nishati.

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi habari wa Brazili João Miranda do Carmo

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO), Irina Bokova, ametoa wito wa kufanyika uchunguzi dhidi ya mauaji ya mwandishi wa habari za mitandao na mhariri João Miranda do Carmo in the Brazilian state of Goiás.

Bokova ambaye amelaani vikali mauaji hayo ameutaka uongozi kuwafikisha wahusika kwenye mkono wa sheria, ili kulinda uwezo wa waandishi wa habari wa kuendelea kuchangia kuelimisha umma.

UN Photo/UNMISS

Uhamishwaji wa wakimbizi kutoka Tomping umeshika kasi

Watu waliosambaratishwa na mapigano ya hivi karibuni ndani ya miji na viunga vyake, wamekimbilia Tomping, Sudan Kusini.

Mafuriko, ukosefu wa mazingira safi na msongamano umelazimu Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini(UNMISS) na Shirika la Uhamiaji(IOM) kuhamisha wakimbizi haowa ndani kutoka Tomping na kuwapeleka Juba.

Katika makala ifuatayo Assumpta Massoi anaangazia harakati hizo..

Naibu mwakilishi wa UNAMID azuru kambi ya wakimbizi wa ndani Darfur:

Naibu mwakilishi wa pamoja wa mpango wa Umoja wa mataifa na muungano wa Afrika wa kulinda amani Darfur UNAMID, Jeremiah Nyamane Kingsley Mamabolo, amezuru kambi ya wakimbizi wa ndani ya Tawilla.

Kambi hiyo iliyoko kaskazini mwa Darfur inahifadhi zaidi ya wakimbizi wa ndani 20,000 wengi wao ni wale waliokimbia kutoka Jebel Marra kufuatia mapigano mpya yam waka huu. Naibu mwakilishi huyo Mamabolo amezuru kambi hiyo kama sehemu ya maadhimisho yam waka wa kimataifa wa vijana. Anaeleza aliyoshuhudia

(SAUTI MAMABOLO)