Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wataalamu wa haki na biashara wa UM kuzuru Mexico

Wataalamu wa haki na biashara wa UM kuzuru Mexico

Pakua

Kikundi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaojishughulisha na mambo ya biashara na haki za binadamu watatembelea nchini Mexico kuanzia Agosti 29 had Septemba 7 mwaka huu.

Ziara hiyo ni kwa ajili ya kuchunguza jitihada za serikali na makampuni tofauti ya biashara ili kuzuia na kushughulikia athari mbaya za haki za binadamu kwenye biashara. Mexico ni nchi kubwa na ya pili katika Amerika ya kusini kuwa na viwanda vikubwa katika sekta mbali mbali ikiwa ni pamoja na umeme, magari na nishati.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa wataalam hao Pavel Sulyanziga. Mtaalam huyo amekaribisha mwaliko wa serikali ya Mexico wa kuendeleza utekelezaji wa taifa wa biashara na haki za binadamu hasa dhidi ya unyanyasaji wa haki za binadamu, biashara, sera na sheria.

Mbali na kukutana na serikali na makampuni mbali mbali makubwa, pia watakutana na raia, watetezi wa haki za binadamu na asasi za kiraia, ameongeza mtaalamu mwingine wa kikundi hicho cha wataalam, Dante Pesce.

Wataalamu hao pia watatembelea majimbo mengine ya Oaxaca, Jalisco na Sonora. Baada ya ziara hiyo watachapisha ripoti na kuiwasilisha kwa Baraza la Haki za Binadamu.

Photo Credit
UN Photo.