Wakimbizi kutoka Sudan wanoingia Sudan Kusini wanaendelea kuongezeka
Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani.
Jifunze Kiswahili: Pata uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “PAMBAJIO”.
Alice Nderitu: Dunia bado haijajifunza lolote kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi
Miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, dunia yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na ukatili wa hali ya juu na mamilioni ya watu kufurushwa makwao. Tangu wakati huo Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele ku
Mariam Suleiman: Wanawake tuna ujuzi, tuna uweo na tunaweza
Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii.
Raia nchini DRC wasimulia jinsi wanavyonufaika na miradi iliyofanikishwa na MONUSCO
Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili ombi la Palestina kuwa mwanachama
Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura.