Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kabrasha la Sauti

© UNICEF/Eyad El Baba

UN: Raia 25, 000 wamepoteza maisha katika vita Gaza na mahitaji ya kibinadamu yanazidi kuongezeka

Mashambulizi makubwa ya mabomu yanayofanywa na Israel Gaza yameendelea tena leo sanjari na maroketi yanayovurumushwa na makundi yenye silaha ya Kipalestina kuelekea Israel, wakati wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakiripoti kuuawa kwa watu zaidi ya 25,000 Gaza tangu kuanza kwa machafuko

Sauti
2'22"
Photo: OCHA Burundi / Ana Maria Pereira

Nchini Burundi mbinu ya mashangazi na baba wa shuleni yaepusha watoto na kejeli kutoka kwa wenzao

Nchini Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kuhakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu bila uoga na jakamoyo hasa pale wanapokumbana na vizuizi vya tofauti ya lugha waliyotumia ukimbizini na ile inayotumika nyumbani

Sauti
2'21"