Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 JANUARI 2024

19 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia vita katika ukanda wa Gaza, na tukielekea siku ya elimu duniani tunabisha hodi nchini Burundi ambako UNICEF inahakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu. Makala na mashinani tunasalia na mada ya elimu bora na tunakupeleka nchini Uganda, kulikoni?.

  1. Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameeielezea hali inayoendelea Gaza siku 105 baada ya kuzuka vita mpya baina ya wapiganaji wa Hamas na vikosi vya Israel, kuwa ni zahma juu ya zahma. Watu zaidi ya milioni 1.7 wametawanywa huku hofu ya milipuko ya magonjwa, janga la njaa na vifo zaidi likitawala. 
  2. Nchini Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kuhakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu bila uoga na jakamoyo hasa pale wanapokumbana na vizuizi vya tofauti ya lugha waliyotumia ukimbizini na ile inayotumika nyumbani walikorejea.
  3. Makala inatupeleka kaskazini mwa Uganda katika wilaya ya Lamwo ambako Kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na ya Uholanzi, Mradi wa Maendeleo wa Kukabiliana na Athari za Ufurushwaji (DRDIP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kutumia mpango wa fedha taslimu wa EmpowerU Cash+ limewasaidia wananchi kuboresha hali yao ya maisha. 
  4. Mashinani Mashinani ttunasalia huko huko Uganda katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali magharibi mwa Uganda kupata ujumbe wa uhusiano wa elimu.      

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'24"