Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali katika ukanda wa Gaza ni zahma juu ya zahma: Mashirika ya UN 

Hali katika ukanda wa Gaza ni zahma juu ya zahma: Mashirika ya UN 

Pakua

Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameeielezea hali inayoendelea Gaza siku 105 baada ya kuzuka vita mpya baina ya wapiganaji wa Hamas na vikosi vya Israel, kuwa ni zahma juu ya zahma. Watu zaidi ya milioni 1.7 wametawanywa huku hofu ya milipuko ya magonjwa, janga la njaa na vifo zaidi likitawala. 

Asante Anold, nikianza na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linaonya juu ya mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza Gaza watu zaidi ya milioni 1.7 waliotawanywa hivi sasa wanaishi katika makazi ya dharura yaliyofurika pomoni na kwa wastani watu 500 wanatumia choo kimoja huku watu zaidi ya 2000 wakitumia bafu moja kuoga na wakati mwingine kwenye baadhi ya makazi ya dharura hakuna choo kabisa.

Hivyo shirika hilo linasema ukosefu wa vyoo na huduma za usafi vimewalazimisha watu kujisaidia haja kubwa kwenye maeneo ya wazi na kuongeza hatari kubwa ya kusambaa kwa magonjwa ya kuambukiza. Tangu katikati ya kwezi Oktoba mwaka jana WHO inasema kumekuwa na makali ya wagonjwa wa kuhara, matatizo ya njia ya mfumo wa hewa, chawa, upele, tetekuanga, homa ya manjano na hata homa ya ini aina ya E.

Osisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR inasema ukiukwaji mkubwa wa haki unaendelea katika ukanda huo mkuu wa ofisi ya haki za binadamu kwenye eneo linalokaliwa la Gaza Ajith Sunghay mbaye yuko Gaza tangu Jumatatu anasema “Nimewaona wanaume na watoto wakifukua vifusi kupata matofali ya kujengea mahema ya mifuko ya plastiki, huli ni janga kubwa la haki za binadamu na janga kubwa lililosababishwa na binadamu. Gaza inahitaji ongezeko la misaada ya kibinadamu ikiwemo ulinzi.”

Kwa upande wake shirika la kuhudumia watoto UNICEF linaangazia watoto wanaozaliwa wakati vita hii ikiendelea, ikiwa ni sikua ya 105 leo shirika hilo linasema karibu watoto 20,000 wamezaliwa katika hali ya jehanamu ikimaanisha mtoto 1 amezaliwa kila baada ya dakika 10 likionya kwamba wengi huenda wakafariki dunia kutokana na vita na hali mbayá ya Maisha na huduma Gaza.

Nahitimisha na Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA ambalo linasema leo ni siku ya tano mfululizo huduma za mawasiliano zimekatwa Gaza na hali hii inazuia maelfu ya watu kupata tarifa za kuokoa maisha, kukosa fursa ya kuwapigia wahudumu wa afya kupata msaada na inaendelea kuathiri usambasaji wa msaada wa kibinadamu unaohitajika sana.

Hadi kufikia sasa kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya ya Gaza takriban watu 25,000 wameuawa tangu Oktoba 7 mwaka jana.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'
Photo Credit
WHO