Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 JANUARI 2024

22 JANUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mradi wa ufugaji nyuki nchini Zimbabwe. Makala tunamuika mkakati wa Afya ya Uzazi kwa Wasichana, Haki, na Uwezeshaji nchini Tanzania na mashinani tunasalia na mada ya elimu bora na tunakupeleka nchini Uganda.

  1. Mashambulizi makubwa ya mabomu yanayofanywa na Israel dhidi ya Gaza yameendelea tena leo sanjari na maroketi yanayovurumushwa na makundi yaliyojihami ya kipalestina kuelekea Israel, wakati wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakiripoti kuuawa kwa watu zaidi ya 25,000 huko Gaza tangu kuanza kwa machafuko hayo mapya Oktoba 7 mwaka jana na mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka kila uchao. 
  2. Nchini Zimbabwe, mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, wa kusongesha ajira rafiki kwa mazingira umeanzisha mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki na hivyo kuandaa vijana kuwa wakulima wajasiriamali vijijini. Mradi huo unatekelezwa kwa ubia na shirika la Korea Kusini la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, KOICA.
  3. Makala inatupeleka nchini Tanzania kuangazia Mkakati wa Afya ya Uzazi kwa Wasichana, Haki, na Uwezeshaji nchini Tanzania (GRREAT) unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau likiwemo shirika lisilo la kiserikali la RLabs Tanzania na serikali ya Canada. Kupitia mpango huu wasichana wamepata zana na ujuzi wanaohitaji ili kuboresha maisha yao, familia na jamii zao. Mmoja wao ni Mariam wa Nyanda za juu kusini mwa Tanzania. 
  4. Mashinani tunakupeleka makazi ya wakimbizi ya Kyangwali magharibi mwa Uganda kupata ujumbe wa uhusiano wa elimu na amani.      

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
10'18"