Surua yavaliwa njuga bara Asia

Mhudumu wa afya akitoa huduma ya jango kwa mtoto huko Bhutan , barani Asia.

Surua yavaliwa njuga bara Asia

03hapanapalewhosuruaasia

Watoto takriban millioni 5 katika kanda ya Kusini-Mashariki ya Asia katika mpangilio wa shirika la afya dunia WHO, kila mwaka hukosa chanjo dhidi ya ugonjwa wa  surua.

Kanda hiyo inazijumulisha nchi sita-Bangladesh, India, Indonesia, Myanmar, Nepal, na Thailand.
Kwa mujibu wa shirika la afya dunianiWHO,  idadi ya watoto wanaokosa chanjo kila mwaka ni kama inadumaza mpango mkakati wa eneo hilo wa kutokomeza sio tu surua lakini pia tetekuwanga na magonjwa mengine yenye asili hiyo.
Kutokana na hali hiyo maafisa wa mipango ya chanjo kutoka nchi hizo pamoja na washirika wao yakiwemo mashirika ya WHO, UNICEF, GVI na mengine wamekutana kwa minajili ya kujadilia changamoto pamoja na uzoefu katika masuala ya chanjo ambazo zinaweza kutumiwa kutokomeza surua pamoja na kudhibiti tetekuwanga ifikapo mwaka 2020.
Mkurugenzi  wa WHO  kanda ya Asia ya Kusini Mashariki, Dkt Poonam Khetrapal Singh  amesema utokomezaji wa surau utafuta  vifo nusu millioni huku kudhibiti tetekuwanga kutaboresha  sio tu afya  kwa mama wajawazito lakini pia watoto wanaozaliwa
Kanda hiyo ina mpango madhubuti wa kuwapa chanjo  dhidi ya  surua na tetekuwanga  takriban watoto millioni 500 wa eneo hilo katika kipindi cha miaka miwili ijayo.