Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2018 waanza na zahma kwa watoto Syria : UNICEF

Mwaka 2018 waanza na zahma kwa watoto Syria : UNICEF

Kwa mujibu wa bwana Fran Equiza, msemaji wa UNICEF Syria, ni masikitiko makubwa kwa wazazi kupoteza watoto mwanzoni mwa mwaka katika miji hii ya mashariki mwa Syria iliyogubikwa na kivita, tangu mwaka 2013 na kuhatarisha maisha ya zaidi ya watoto wengine laki mbili.

Mkuu huyo wa UNICEF amesema katika mji wa Idlib ulioko kazikazini kumeripotiwa mapigano mapya  hivi karibuni na kusababisha vifo, mejeruhi na ukimbizi wa ndani kwa zaidi ya watu laki moja wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Katika ripoti yake bwana Equiza amesema wamepokea pia taarifa ya   mashambulizi ya hospitali mbili huko mashariki mwa Ghouta ambapo wahudumu wanaripotiwa kufunga huduma  za afya, na shule kutokana na ukosefu wa usalama .

UNICEF imesema itaendelea kutoa huduma huko Syria haswa kwa watoto na wanawake ambao ni wahitaji wakubwa katika migogoro, japo mazingira ya usalama ni hatarishi kwa wafanya kazi wake na pia mashirika mengine  ya kibinadamu.