Baraza la Usalama la UM limelaani vikali shambulio dhidi ya MINUSMA
Wajumbe wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mashambulizi dhidi ya vikosi vya walinda amani vya ujumbe wake Mali (MINUSMA) katika eneo la Ménaka, lililofanyika Novemba 24, 2017, na kusababisha vifo vya askari 3 kutoka Nigeria, na kujeruhiwa wengine 21.
Wajumbe wa baraza la usalama wametuma salamu zao za rambirambi kwa familia za wafiwa, serikali ya Nigeria na pia ujumbe wa MINUSMA huku wakiitaka mamlaka ya Mali kuchukua hatua za kisheria ili kuhakikisha wahusika wanatiwa nguvuni na vyombo vya dola.
Aidha wajumbe wasema kamwe hawatafumbia macho vita dhidi ya ugaidi kwa njia zozote na kuahahakikisha unakomeshwa kabisa na pia wamezitaka serikali zote duniani kushirikiana katika vita dhidi ya mitandao yote ya kigaidi kwa nguvu zote.
Pia wamesema ni lazima kuiwezesha MINUSMA katika kuhahakisha wanapata vitendea kazi kwa mujibu wa Azimio la Baraza la Usalama 2364 (2017) ili kuweza kujilinda na pia kulinda maeneo wanayoyahudumia huko Mali na sehemi nyingne.