Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa haki za binadamu ziarani Mali kufuatia taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu

Mtaalam huru wa maswala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Suliman Baldo. Picha: UM/Jean-Marc Ferré

Mtaalamu wa haki za binadamu ziarani Mali kufuatia taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu

Mtaalam huru wa maswala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Suliman Baldo anatarajia kuanza ziara ya kikazi  Mali kuanzia tarehe 27 Novemba hadi 1 Desemba 2017, kutokana na taarifa ya ucheleweshaji unaoendelea katika utekelezaji wa makubaliano ya amani ya nchi humo.

Bwana Baldo amesema kuna taarifa ya ukiukwaji wa haki za binadamu mkubwa nchini mali  haswa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya  wanawake, pamoja na kuwa mamlaka ya Mali ilisaini makubaliano ya amani  na upatanisho mwezi juni mwaka 2015.

Aidha bwana Baldo amsema ucheleweshwaji katika kutekelezaji wa mkataba huo unaifanya mamlaka ya  Mali kukosa kusimamia haki za binadamu husani maeneo ya kazikazini mwa Mali ambako unyanyasaji wa kisijinsia unakithiri kwa wanawake.

Akiwa ziarani nchini humo Bw. Baldo atatembelea ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA na pia ofisi za haki za binadamu ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo Mali.