Nchi zachukua hatua kupambana na usugu wa vijiumbe maradhi: FAO

17 Novemba 2017

Juhudi za kimataifa za kupambana na kuenea kwa usugu wa vijiumbe maradhi mashambani na kwenye mfumo wa chakula zina shika kasi , kutokana na kuungwa mkono na serikali na msaada wa kiufundi unaoziwezesha nchi kukabili tatizo hilo limesema shirika la shakula na kilimo FAO hii leo.

Limeongeza kwamba dawa za vijiumbe maradhi zinatumika kwa kiasi kikubwa katika mifugo, kuku na ufugaji wa samaki ili kuzuia magonjwa lakini matumizi mabaya na  ya kupindukia ya dawa hizo kwa afya ya binadamu na wanyama , yanachangia hali ya dharura na kusambaa kwa magonjwa na hivyo kusababisha usugu ambao inakuwa vigumu kutibika tena na viuavijasumu au antibiotics.

Utafiti wa kwanza wa kila mwaka uliofanywa na FAO,  shirika la kimataifa la afya ya mifugo OIE, na shirika la afya ulimwenguni WHO mwaka 2016,  umebaini kwamba kuna hatua zinazochukuliwa kukabiliana na tatizo hilo na zaidi ya watu bilioni 6.5 au asilimia 90 ya watu wote duniani wanaishi katika nchi ambazo tayari zina mipango ya kitaifa kuchukua hatua inayojumuisha afya ya binadamu na ya wanayama.

Kenya ni miongoni mwa nchi 12 Afrika na Asia zinazoshiriki mradi wa FAO unaofadhiliwa na Uingereza wa kuzijengea nchi uwezo wa kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya hatari za usugu wa vijiumbe maradhi katika chakula na kilimo.