Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa kuadabisha watoto majumbani ni mwiba kwa watoto - UNICEF

Mfumo wa kuadabisha watoto majumbani ni mwiba kwa watoto - UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNCEF limetoa ripoti mpya  ya kuhusu unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto ikiwa ni uchunguzi wa kina katika masuala ya ukiukwaji wa haki za msingi za mtoto.

Claudia Cappa  ambaye ni mtaalamu wa takwimu wa UNICEF na mwandishi wa ripoti hiyo amesema wamebaini watoto wananyanyaswa shuleni,  nyumbani na mara nyingi wanafanyiwa vitendo hivyo na watu ambao wana wajibu wa kuwalea.

(Claudia Clappa )

“Ripoti inabainishia kuwa robo tatu ya watoto wenye umri wa kati ya miaka miwili hadi minne hukumbwa na unyanyasaji wakati wanaadabishwa na walezi wao majumbani. Ukatili huu ni kama vile kuchapwa viboko au  kisaikolojia ambavyo hutumiwa na walezi na pia wazazi kila siku. Matukio haya huwaathiri watoto wenye umri wa hata miezi 12. Takribani asilimia hamsini ya watoto wenye umri wa mwaka mmoja hukabiliwa na adhabu ya viboko au ukatili wa kisaikolojia kutoka kwa walezi wao.

Ameongeza kuwa ripoti hiyo imetaja watoto wengine duniani ambao wameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na vitendo wanavyofanyiwa jamaa au wazazi wao.

(Claudia Cappa)  

“Ulimwenguni kote watoto wapatao milioni 176 duniani wenye umri wa chini ya miaka mitano wameripotiwa kuishi na mama ambao  wanakabiliwa na ukatili kutoka kwa wapenzi wao. Watoto wanakabiliwa pia na ukatili shuleni ambapo wananyanyaswa na wenzao na hii inaathiri karibu watoto milioni 130 wenye umri wa kwenda shule duniani kote.”

image
Watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakicheza ikionyesha kuwa wana furaha. (Picha:Amanda Nero I IOM 2017)