Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo kutokana na TB yapungua, Tanzania nayo yachukua hatua

Idadi ya vifo kutokana na TB yapungua, Tanzania nayo yachukua hatua

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO inaonyesha kuwa ingawa idadi ya vifo kutokana na ugonjwa wa Kifua Kikuu au TB ilipungua mwaka jana, bado ugonjwa huo ni tishio. Selina Jerobon na ripoti kamili.

(Taarifa ya Selina)

Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka jana watu milioni 1.3 walifariki dunia ulimwenguni kutokana na ugonjwa huo, ikiwa ni pungufu kwa vifo Laki Nne ikilinganishwa na mwaka 2000.

WHO inasema bado TB ambao bado unashika namba ya tisa kwa kusababisha vifo duniani, unaweza kutokomezwa kwa uchunguzi wa mapema na mgonjwa kupatiwa tiba mahsusi.

Nchini Tanzania,  Dkt Liberate Mleoh ambaye ni meneja msaidizi wa mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma nchini humo anasema changamoto nchini humo ni kuibua wagonjwa wapya lakini hivi sasa wameibuka na mkakati mpya...

(Sauti ya Dkt. Mleoh)

Amesema sambamba na mkakati huo idadi ya maaabara za kupima TB zimeongezeka tofauti na awali ambapo ilikuwa lazima mgonjwa aende hospital ya Kibong’oto mkoani Kilimanjaro.

(Sauti ya Dkt. Mleoh)

image
Watendaji wa mradi wa taifa wa TB na Ukoma nchini Tanzania wakifuatilia rejesta za wanaohisiwa kuwa na ugonjwa wa TB nchini humo. (Picha:kwa hisani ya MoHSW NTLP)