Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto kushika hatamu ya uongozi siku yao tarehe 20 mwezi ujao

Watoto kushika hatamu ya uongozi siku yao tarehe 20 mwezi ujao

Wiki chache zikiwa zimesalia kuelekea maadhimisho ya siku ya mtoto duniani, yenye kaulimbiu “ shika nafasi”, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limesema mamilioni ya watoto ulimwenguni kote watatumia siku hiyo kufanya kazi mbalimbali katika sekta wazipendazo.

 
UNICEF imesema tarehe hiyo ya 20 Novemba  ni kumbukumbu ya kupitishwa kwa mkataba wa haki za mtoto, CRC unaotaja haki kuu nne za msingi za mtoto ambazo ni kuishi, kuendelezwa, kushirikishwa na kulindwa.
 
Kwa mantiki hiyo watoto watajumuika kuongoza shughuli mbalimbali kama katika sekta ya habari, michezo, biashara na kadhalika.
 
Naye balozi mwema wa UNICEF David beckham atapewa nafasi ya kuwauliza maswali watoto kuhusu filamu fupi itakayozindiliwa siku  ya watoto duniani huku naye David Villa mwanasoka wa Hisptania anayechezea klabu ya New  York atazungumza na watoto kuhusu masuala ya serikali.
 
UNICEF imesema watoto watatumia jukwaa hilo kuelezea vikwazo na matatizo yanayowakabili katika maisha yao ya kila siku kama vile unyanyasaji na ubaguzi.
 
Ikumbukwe tu kwamba watoto milioni 385 wanaisha katika u