Usafiri wa meli na bandari vina mchango mkubwa katika SDG’s:IMO

28 Septemba 2017

Katika kuadhimisha siku ya masuala ya bahari duniani , shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya bahari IMO limesema usafiri wa meli na bandari vina mchango mkubwa katika kutatua tatizo la ajira na kuimarisha biashara.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni “muungano wa meli, bandari na watu, kama anavyofafanua Katibu Mkuu wa IMO Kitack Lim kauli mbiu hiyo ina umuhimu wake kwani

(sauti ya KIM)

“Itatuwezesha kutanabaisha ushirikiano uliopo baina ya bandari na meli ili kudumisha na kuimarisha mfumo salama na wenye ufanisi wa usafiri wa bahari.”

Ameongeza kuwa sekta ya bahari ambayo inajumuisha usafirishaji, bandari na watu inaweza kuwa chachu kubwa ya kufanikisha malengo ya maendeleo au SDG’s

(Sauti ya Kim)

Kama shirika la Umoja wa Mataifa, IMO ina wajibu mkubwa wa kusaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Usafirishaji wa meli na bandari unaweza kuwa na jukumu muhimu la kuweka mazingira ya kupanua wigo wa ajira, kuleta mafanikio na ufanisi kwa kuchagiza biashara ya  masuala ya bahari. Bandari na bahari vinaweza kuwa vyanzo vya utajiri kwa nchi kavu na baharini.”

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter