Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tutapataje amani kama twawekeza kwenye silaha? – Mugabe

Tutapataje amani kama twawekeza kwenye silaha? – Mugabe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amehoji ni amani inaweza kufanikiwa duniani ilhali serikali zinawekeza kila uchao kwenye silaha.

Ametoa hoja hiyo wakati akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani siku ya Alhamisi akisema ni dhahiri kuwa mtu huvuna kile anachopanda.

(Sauti ya Mugabe)

“Katika ajabu na kweli, tunatarajia kuvuna amani wakati tunawekeza katika teknolojia ya vita. Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2016 matumizi ya kijeshi duniani yalifikia dola trilioni 1.6. Wakati huo huo usaidizi wa kigeni wa maendeleo ulikuwa zaidi ya dola bilioni 142.5. Uwekezaji huo mkubwa kwenye silaha za sumu na silaha za kisasa haujaleta amani na badala yake tumeshuhudia machungu na idadi kubwa ya watu wakikimbia mizozo na vita. Mweleko huu ukomeshwe kwa maslahi ya binadamu.”

Kuhusu maendeleo endelevu, Rais Mugabe amesema ajenda hiyo ni ya aina yake akiitaja kuwa ni ya kimapinduzi na yenye kuonyesha matumaini makubwa lakini amesema..

(Sauti ya Mugabe)

“Kwa sisi Afrika, mfumo wa kimataifa hivi sasa ni wa kizamani na ni dhihirisho la historia ya ukosefu wa haki ambao kamwe hakuna anayeweza kuuhalalisha hivi sasa. Ajenda ya 2030 inawakilisha mvinyo mpya na sisi tunataka chupa mpya ya kubebea ili tusiharibu huu mvinyo.”