Umoja wa Mataifa utekeleze majukumu bila upendeleo- Kagame

20 Septemba 2017

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiingia siku ya pili, Rais Paul Kagame wa Rwanda ametaka chombo hicho kitekeleze majukumu yake bila kuegemea upande wowote.

Akihutubia viongozi wa nchi wanachama, Rais Kagame amesema ingawa kila mwaka Umoja wa Mataifa unatumia mabilioni ya fedha kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kule kwenye majanga, bado kuna hisia kwamba chombo hicho hakikidhi mahitaji na matarajio ya wanachama.

Amesema ni kwa mantiki hiyo Rwanda inaunga mkono hatua za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa za kuleta marekebisho ya muundo wa chombo hicho sambamba na kuhakikisha kuna uwajibikaji akisema..

“Ili kuweza kuwa na ufasini katika kufanikisha azma yamaisha yenye hadhi kwa wote, Umoja wa Mataifa lazima uhudumia watu wote kwa heshima na bila upendeleo na ni lazima utunze vyema fedha zinazopatiwa dhamana ya kutumia.”

Rais Kagame ni miongoni mwa mabingwa wa kusongesha usawa wa kijinsia ambapo alipoulizwa na idhaa hii baada ya hotuba ni kitu gani kinaleta mafanikio hayo, amesema..

(Sauti ya Kagame)

“Tunajaribu kufanya mambo katika mwelekeo ambao unaeleweka, vile ambavyo unafikiri vinapaswa kufanyika. Ni kuweka fikra zako katika kile ambacho unataka kufanya.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter