Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana na jukumu lao katika amani na maendeleo

Vijana na jukumu lao katika amani na maendeleo

Nguvu kazi ya taifa, taifa la leo, taifa la kesho! Ni baadhi ya kauli ambazo hutumika ili kuchagiza kundi hilo ambalo linatagemewa kwa maendeleo kwani idadi yake kwa sasa nikubwa kabisa katika historia ya dunia. Takwimu kwa sasa zinaonyesha kuwa vijana ni zaidi ya bilioni 1.8.

Kundi hili linakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwamo ukosefu wa ajira.

Kila mwaka mnamo tarehe 12 Agosti, dunia huadhimisha siku ya vijana, ambapo pamoja na mambo mengine, siku hii huzimuika changamoto kwa kundi hilo na namna ya kuzitatua. Katika maadhimisho hayo mwaka huu, Umoja wa Mataifa umetoa ujumbe wa kuwashirikisha vijana hususani katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu, ikiwa ni sehemu ya maudhui ya mwaka huu ambayo ni Kujenga Amani.

Katika muktadha huo, vijana kutoka sehemu mbalimbali duniani walikusanyika hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kuhudhuria mkutano wa baraza la vijana ambalo lilijadili chagamoto, zikabilizo kundi hilo na kujikita zaidi katika namna ya kutekeleza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu SDGs. Mwenyeji wao alikuwa ni Jayathma Wickramanayake, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa umoja huo kuhusu vijana.

Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Joseph Msami ……….

( Sauti Jayathma Wickramanayake)

‘‘Zaidi ya vijana milioni 600 wanaishi katika maeneo tete au yenye machafuko. Na zaidi ya vijana milioni 400 hawapati huduma muhimu za afya. Hili lazima libadilike. Tuko tayari kufanya kazi na vijana na kwa ajili yao ili kuzitambua na kuzishikilia haki zao pamoja na kupigia chpeo uraia wao wa kimataifa.’’

Katika kuzimulika changamoto ziwakabilizo vijana katika sehemu mbalimbali, ikiwamo amani na maendeleo, John Kibego wa idhaa hii amezungumza na kijana Edson Nzeimana ambaye ni mwanafunzi kutoka DRC anayepata usaidizi kutoka kambi ya wakimbizi nchini Uganda, baada ya kufurushwa.

( Sauti Edson)

image
Vijana waliohudhuria mkutano wa vijana kutoka Kenya, Moureen Ngoro na Winnie Michaels. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili
Tukijerea hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa,ambapo mijadala ya vijana ilijiri, Joseph Msami amepata fursa ya kuzungumza na moja ya vijana waliohudhuria mkutano huo kutoka Kenya, Moureen Ngoro na Winnie Michaels awali anazungumza na Moureen ambaye ni mlimbwende wa Miss Utalii kutoka kaunti ya Nyamira.