Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wajumuishwe kuleta maendeleo: Jayathma

Vijana wajumuishwe kuleta maendeleo: Jayathma

Wakati siku ya kimataifa ya vijana ikiadhimishwa kote duniani Agosti 12, hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, leo vijana kutoka pembe mbalimbali za dunia wamejadili umuhimu wa kukabiliana na umaiskini na ujumishwaji pamoja mazingira. Flora Nducha na taarifa kamili.

(TAARIFA YA FLORA)

Vijana hao wanaowakilisha kundi hilo linalokadiriwa kuwa bilioni 1.8 kote duniani, wamejadili namna ya kukabili umasikini, na umuhimu wa kujenga uchumi unayojali mazingira.

Wazungumzaji wamehamasisha umuhimu wa ujumuishwaji wa vijana katika maendeleo hususani utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 yaani SDGs.

Awali katika mahojiano maalumu na redio ya Umoja wa Mataifa, mwakilishi maalum mpya wa vijana Jayathma Wickramanayake amezungumzia umuhimu wa kuwajumuisha vijana katika ajenda ya maendeleo endelevu akisema

( Sauti Jayathma)

"Kuna haja ya Umoja wa Mataifa kuwashirikisha vijana na kupata mtazamo wao wa jinsi dunia inavyopaswa kuwa ifikapo mwaka 2030, kwani hatimaye ni vijana hawa ambao wataongoza utekelezaji wa ajenda hii, kwa hiyo nafikiri wakati huu ni wakati wa kihistoria wa kuleta mabadiliko".