Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka 100 ya kristalografia imeleta maendeleo ya sayansi: Ban

Miaka 100 ya kristalografia imeleta maendeleo ya sayansi: Ban

Mwaka 2014 umetajwa kuwa ni mwaka wa kimataifa wa Kristalografia ambayo ni elimu ya sayansi kuhusu mada. Ikiwa ni miaka 100 tangu ugunduzi wa sayansi hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametuma ujumbe wake akieleza kuwa Kristalografia imeleta mapinduzi makubwa katika sayansi za afya, kilimo na hata bayoteknolojia.

Hii leo, Kristalografia ni moja ya misingi ya miundo ya sayansi, ikidhihirisha muundo wa madini, molekyuli za uhai, ikisaidia wanasayansi kubuni mambo mapya ikiwemo tiba za kuokoa maisha.”

Bwana Ban amesema kwa kutambua umuhimu wa mchango wa Kristalografia , Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limetenga mwaka 2014 kuwa mwaka wa kimataifa wa kristoligrafia.

Amesema lengo ni kuongeza uelewa wa jamii juu ya umuhimu wa maada, kuimarisha ushirikiano na kujenga ubia mpya duniani kote juu ya sualahilo.

Tovuti ya kuadhimisha mwaka huo, www.iycr2014.org  imetolea mfano kampuni za kutengeneza dawa ambazo iwapo zinatafiti dawa ya kudhibiti aina ya kimelea, ni lazima ifahamu umbo la molekyuli inayoweza kuzuia vimeng’enya au enzymes ambazo zinashambulia seli ya binadamu na hiyo  imerahisishwa na Kristalografia .