Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid ateua tume kutathimini hali ya Kasai DRC

Zeid ateua tume kutathimini hali ya Kasai DRC

Wakati baraza la usalama limekutana hii leo kujadili hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC kamishina Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein ametangaza uteuzi wa Bacre Ndiaye kutoka Senegal, Luc Côté kutoka Canada, na Fatimata M’Baye kutoka Mauritania kama jopo la kimataifa la wataalamu kutathimini hali ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Grace Kaneiya na taarifa kamili

(TAARIFA YA GRACE)

Bacre Ndiaye atakuwa mwenyekiti wa tume hiyo iliyoundwa kwa mujibu wa azimio la baraza la haki za binadamu lililopitishwa Juni 22 mwaka huu. Azimio hilo lilianisha hofu kuhusu hali nchini DRC hususani katika majimbo ya Kasai ikijumuisha machafuko, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa .

Ukiukwaji huo ni pamoja na kuingizwa watoto jeshini, ukatili wa kingono, upatikanaji wa makaburi ya pamoja, ukatili wa kijinsia, uharibifu wa makazi, shule, nyumba za ibada na miundombinu ambao unaofanywa na makundi ya wanamgambo. Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(RAVINA CUT)

“Timu hiyo imepewa jukumu la kukusanya taarifa ili kubaini ukweli na mazingira yaliyochangia ikiwa ni pamoja na kuzuru maeneo kunakodaiwa kutendeka ukiukwaji huo , hivyo tunategemea ushirikiano wa serikali ya DRC kuwezesha ziara hizi na fursa ya kuingia nchini, kwenye maeneo husika na kwa watu husika. Na pia ni muhimu sana kwa serikali kuelewa kwamba timu hii ya wataalamu imepewa jukumu la kuangalia ukiukwaji uliotendeka bila kujali nani ameutenda”

Kamishina Mkuu Zeid ana mpango wa kuwasilisha ripoti hali ya Kasai kwa baraza kuu la haki za binadamu mwezi Machi mwaka ujao.