Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amani na demokrasia ndio misingi ya kujenga upya DRC-Amina

Amani na demokrasia ndio misingi ya kujenga upya DRC-Amina

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina J. Mohammed yuko ziarani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, DRC kama sehemu ya ziara yake Afrika. John Kibego na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JOHN)

Bi Mohammed akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano na wanawake viongozi amesema uwepo wake nchini humo ni kiashiria cha umhuhimu wa kuona taswira ikibadilika kuhusu janga linaloshuhidiwa nchni DRC la ukatili na hususan dhidi ya wanawake na watoto, huku akisisitiza umuhimu wa kuwashirikisha wanawake katika kukabiliana na changamoto zinazokabili nchi hiyo.

(Sauti ya Amina)

“DRC ni nchi ya kipekee na kwamba ina katiba na sheria, lakini ni lazima sheria hizo zitekelezwe ili kushirkisha wanawake na mchango wao, mchango wa wanawake kwa kiasi kikubwa katika nafasi za kufanya maamuzi, na fursa za kushiriki katika kusimamia uchaguzi jumuishi na huru, na kwamba upinzani una nafasi yake kwa sababu katika kila demokrasia, vyama vya upinzani thabiti ni kielelezo cha uadilifu na ni matumaini ya kuimarisha misingi ya demokrasia.”

Ameongeza kwamba ili kutatua changamoto nchini DRC cha muhimu ni..

“Amani ndio nguzo ya kusaidia kufikia uwezo wetu na kuhakikisha kwamba haki za bindamu zinaheshimiwa na hapa tunaona kwamba haki za wanawake ambazo ni haki za bindamu hazizingatiwi na safari ni ndefu,tukiangazia ukatili wa kijinsia hatua zimepigwa kwani sasa kiongozi anayesimamia hilo ni mwanamke lakini kile tunachotaka kuona ni visa sufuri vya ukatili wa kijinsia.”