Ubunifu katika afya waleta nuru Afrika

Ubunifu katika afya waleta nuru Afrika

Jukwaa la kwanza la afya barani Afrika limeanza kikao chake cha siku mbili huko Kigali, Rwanda ambapo ubunifu katika kupatia suluhu magonjwa linapatiwa kipaumbele.

Mkuu wa ofisi ya shirika la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti akifungua jukwaa hilo amesema ubunifu na afya mtandao vinasaidia kubadilishana taarifa kati ya watoa huduma na wahudumiwa akipongeza nchi ambazo zimepitisha sera kutumia mbinu hiyo.

Uganda ni mojawapo ya nchi ambapo Waziri wake anayehusika na afya Dkt. Sarah Opendi ameweka bayana jinsi teknolojia hiyo inavyoleta manufaa..

(Dkt. Opendi)

“Tuna jopo la wahandisi wanawake, AfriGal waliogundua mbinu ya Mndex ambayo inaweza kubaini selimundu, ugonjwa ambao sasa ni changamoto kubwa nchini mwetu. Mbinu nyingine iliyobuniwa ni ile ya kubaini Kifua Kikuu-TB.”

Maudhui ya jukwaa hilo ni Kupatia watu kipaumbe;Mwelekeo wa afya kwa wote barani Afrika ambapo WHO kanda ya Afrika imepigia pia chepuo huduma ya chanjo kwa watoto kama mbinu muhimu zaidi ya kulinda watoto dhidi ya magonjwa.