Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Safari ni ndefu lakini kuna matumaini kutokomeza madawa ya kulevya- Guterres

Safari ni ndefu lakini kuna matumaini kutokomeza madawa ya kulevya- Guterres

Kwa pamoja ni lazima tutimize ahadi ya wote ili kupunguza biashara, matumizi na madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kwenye ujumbe wake kwa siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya madawa ya kulevya inayoadhimishwa kila Juni 26.

Guterres amesema, kwa uzoefu wake anafahamu jinsi tahadhari na tiba vinaweza kuleta matokeo mujarabu akitolea mfano nchi yake Ureno wakati alipokuwa waziri mkuu ambako kwa sasa ni nchi yenye idadi ndogo ya vifo vinavyotokana na matumizi ya mihadarati bara Ulaya.

Licha ya changamoto zinazokabili utatuzi wa tatizo hilo la kimatifa, Katibu Mkuu huyo amesema anatumai na kuamini kwamba dunia iko katika njia sahihi na kwa pamoja kuna uwezekano wa kutekeleza mbinu muafaka ambazo zitazaa matokeo endelevu.