Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wavuvi walalama kipato kidogo Tanzania

Wavuvi walalama kipato kidogo Tanzania

Mkutano wa kimataifa kuhusu bahari ukifikia tamati hii leo, nchini Tanzania wavuvi kutoka mkoani Tanga, wameesema kuwa sababaui kadhaa zikiwamo mabadiliko ya tabanchi zimesababaisha kupungua kwa samaki katika bahari ya Hindi.

Katika mahojiano na Maajabu Ally wa redio washirika Pangani Fm ya mkoani humo, wavuvi hao Rajabu Madaraka na Ali Mkada wamesema juhudi zaidi za serikali zinahitajika ili bahari iwanufaishe zaidi wavuvi na jamii kwa ujumla.

( Sauti Wavuvi)