Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhifadhi wa mazingira hususan Afrika

Uhifadhi wa mazingira hususan Afrika

Mapema juma hili, dunia imeadhimisha siku ya mazingira, siku ambayo huadhimishwa Juni tano ya kila mwaka. Ujumbe wa mwaka huu ni utengamano na asili, ukilenga kuhakikisha ulinzi wa maliasili za mazingira ili kukuza uendelevu wa viumbe na sayari dunia.

Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP na wadau  wake,  wametumia maadhimisho hayo kufikisha ujumbe juu ya  kuithamini dunia kwa kulinda mazingira dhidi ya changamoto za uharibifu.

Maliasili kama vile bahari ,ardhi, misitu , maji na hewa ivutwayo na viumbe hai vimepigiwa chepuo kulindwa ili kuhakikisha sayari hiyo inabaki salama kwa kizazi cha sasa na vijavyo.

Sasa barani Afrika ni hatua gani zinachukuliwa? Tuanzie nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo DRC na Langi Stan Asumani wa redio washirika Umoja redio ya jimboni Kivu Kusini ambaye amezungumza na wanamazingira Esombola Chimbalanga na Asan Jerad (Jheraad) wanaofafanua jinsi gani shughuli za kila siku mathalani mapishi na zile za kimaendeleo huharibu mazingira.