Mkutano kwa ajili ya Syria ukianza , UM waonya dhidi ya ukataji ufadhili
Wakati mkutano mkubwa wa kimataifa umeanza leo mjini Brussels Ubelgiji, mashirika ya Umoja wa mataifa yameonya kwamba kudorodra kwa msaada wa fedha kutoka nchi wanachama kutauweka njia panda msaada muhimu kwa mamilioni ya wakimbizi wa Syria na jamii zinazowahifadhi.
Ameongeza kuwa dunia bado ina fursa ya kuonyesha mshimakano na watu walio katika madhila, kuwasaidia , binafsi, bila ubaguzi, kisiasa, na bila masharti yoyote ili kuokoa maisha yao popote walipo, kwa njia yoyote na wakato wowote.
Amesema wanawashukuru wote waliojitolea hadi sasa lakini ukweli ni kwamba ufadhili hauendi sanjari na mahitaji, na watu milioni 13.5 wanaume, wanawake na watoto ndani ya Syria wanahitaji msaada wa haraka. Watu wengine zaidi ya milioni 5 ni wakimbizi nchi jirani za Misri, Iraq, Jordan, Lebanon na Uturuki ,huku wengine kwa maelfu wamefanya safari za hatari kwenda Ulaya na kwingineko kukimbia vita.
Chakula na msada wa fedha taslimu vitapunguzwa au kukatwa kabisa katikati ya mwaka huu na kuongeza changamoto za utulivu na usalama katika ukanda mzima.
Ameongeza kuwa hadithi katika eneo zima ni ilele huduma za maji na usafi, ajira na soko la nyumba vyote viko katika hatihati.
Amesema inganwa UNDP na wadau wako huko kusaidia masuala ya miundombinu, kuboresha maisha ya watu na kuleta maendeleo katika jamii lakini mahitaji ni makubwa na msaada unahitajika haraka.
Mkutano huo utaendelea Jumatano ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kuhutubia.