Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria ondoeni vikwazo vya kiutendaji ili misaada ifike- UM

Syria ondoeni vikwazo vya kiutendaji ili misaada ifike- UM

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo wamepokea taarifa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Syria ambapo wameelezwa kuhusu vizuizi vinavyoendelea kukwamisha misafara iliyobeba misaada ya kibinadamu.

Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Machi, Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ameeleza hayo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao kilichohutubiwa na mkuu wa masuala ya usaidizi wa dharura kwenye Umoja wa Mataifa Stephen O’Brien. Balozi rycroft amesema..

(Sauti ya Balozi Rycroft)

“Tumejadili umuhimu wa kubadilisha hatua za kufikia maeneo magumu zaidi kufikika ili kutekeleza kwa ukamilifu mpango wa misafara ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake. Na kwa mantiki hiyo tunatoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vyovyote vya kiutendaji”

Wajumbe pia wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha sitisho la mapigano nchini kote Syria ili kuweza kufikisha misaada ya kibinadamu.