Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mdudu hatari anayeshambulia minazi na mitende aleta changamoto- FAO

Mdudu hatari anayeshambulia minazi na mitende aleta changamoto- FAO

Mdudu hatari alaye mimea ya minazi na tende amesababisha shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kuitisha mkutano wa siku tatu huko Roma, Italia ili kujadili mpango wa kimataifa wa kuzuia kuenea kwake hususan Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini.

FAO imesema mkutano huo utakaoutanisha wanasayansi, wataalamu wa kudhibiti wadudu, mawaziri wa kilimo na wakulima utaweka mikakati dhidi ya mdudu huyo ambaye asilimia 80 ya mzunguko wake wa maisha ni ndani ya shina la mti, siyo dhahiri kuonekana na kudhibitiwa.

Shoki Al Dobai, Afisa wa Kikanda wa Ulinzi wa Mazao, FAO, amesema hili ni janga ambalo linasababisha nchi husika zinazotumia minazi kama vile ya mapambo, kupoteza dola milioni 8 kwa mwaka kudhibiti usambaaji wake, ilhali pia wakulima wanapoteza kipato, na hatari zaidi ni kwa afya kwani..

(Sauti ya Al Dobai)

"Kwa matumizi makubwa ya viuatilifu kudhibiti wadudu hawa, kama mnavyojua minazi ya mapambo hupandwa barabarani, katika bustani, majumbani na wakati mwingine karibu na shule, hospitali na kadhalika".