Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO na mkakati wa kupunguza madhara ya makosa ya matumizi ya dawa

WHO na mkakati wa kupunguza madhara ya makosa ya matumizi ya dawa

Shirika la afya ulimwenguni WHO kupitia kitengo chake cha kimataifa cha usalama na changamoto kwa mgonjwa, linanuia kukabiliana na madhaifu katika mfumo wa afya ya makosa katika matumiziya dawa yanayosababisha madhara kwa watumiaji.

Grace Kaneiya na taarifa zaidi.

( TAARIFA YA GRACE)

WHO katika maelezo yake inasema marekebisho ya mfumo huo yanalenga kuimarisha matumizi ya dawa zitolewazo kwa maelekezo ya wataalamu wa afya, namna zinavyosambwazwa na hivyo kuongeza uelewa kwa wagonjwa kuhusu athari za matumizi yasiyo sahihi ya dawa.

Takwimu kwa bara la Amerika pekee, zinaonyesha kuwa makosa ya matumizi ya dawa husababisha kifo cha anagalau mtu mmoja kila siku na kujeruhi watu milioni 1.3 kwa mwaka huku kiwango hicho kiitarajiwa pia katika nchi zenye kipato cha kati na kidogo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk Margaret Chan, amenukuliwa akisema kuwa kila mtu hutarajia kusaidiwa na sio kuangamizwa anapotumia dawa, na kwamba kuepuka makosa ya dawa kutaokoa fedha na maisha.