Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda, Kenya zimepiga hatua katika kuwawezsha wanawake:Mawaziri

Uganda, Kenya zimepiga hatua katika kuwawezsha wanawake:Mawaziri

Kikao cha ngazi ya mawaziri kilichoangazia uwezeshaji wa wanawake na uhusiano wake katika malengo ya maendeleo endelevu SDGs, kimefanyika hii leo ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 61 tume ya hadhi ya wanawake CSW61 unaondelea mjini New York, Marekani.

Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wamehutubia kikao hicho akiwamo waziri wa jinsia ,kazi na maendeleo ya jamii wa Uganda Janat Mukwaya, katika hotuba yake amesema serikali imeweka mkakati wa kisheria unaohakikisha usawa na kupinga ubauzi katika maeneo ya kazi.

Amesema sheria za kazi zimekuwa na umuhimu katika kukuza ushiriki wa wanawake katika soko la ajira nchini Uganda akitolea mfano wa sheria ya ajira ya mwaka 2006 inayouzuai unyanyasaji na ukatili wa kingono

Bi Mukway amefafanua kuwa sheria hiyo inaruhusu likizo za uzazi kwa akina baba na akina mama, inayosaidia maendeleo ya mtoto na afya ya uzazi na haki pamoja na kumpunguzia mama majukumu ya ulezi.

Kwa upande wake Waziri wa huduma za umma, vijana na masuala ya wanawake Sicily K. Kariuki amesema licha ya changamoto kadhaa hatua kubwa katiak kuwawezesha wanawake zimepigwa akitolea mfano wa mipango ya upatikanaji wa mikopo na samani zisizohamishika ambapo takribani wanawake milioni tatu wamenufaika.

Akitolea mfano amesema sera ya elimu ya bure, elimu ya sekondari inayogharimiwa ruzuku na hatua za kijinsia katika kuongeza usajili wa wanawake katike elimuya juu. Wanawake wawili kati ya watatu walio katika umri kati ya miaka 25 na 35 wamehitimisha angalau shule ya sekondari.

Bi Kariuki amesema katika mausuala ya uongozi na uamuzi, taifa hilo lina katiba inayohakikisha theluthi ya uwakilishi wa jinsia zote katika nafazi za kuchaguliwa na kuteuliwa.