Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna pengo la mishahara baina ya wanawake na wanaume Tanzania: Kigwangalla

Hakuna pengo la mishahara baina ya wanawake na wanaume Tanzania: Kigwangalla

Serikali ya Tanzania imesema injivunia hatua zilizopigwa katika suala la ukombozi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwemo kisheria, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto, Dr Hamisi Kigwangalla alipohojiwa na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani kinachoendelea kwenye Umoja wa Mataifa.

Akigusia moja ya changamoto kubwa za kimataifa kuhusu pengo la asilimia 23 katika mishahara baina ya wanaume na wanawake amesema

(KIGWANGALA CUT 1)

Na kuhusu kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu kwa upande wa wanawake amesema serikali imelivalia njuga na ina mikakati kabambe

(KIGWANGALLA CUT 2)