Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana hawakumbatii ubaguzi bali mshikamano-Guterres

Vijana hawakumbatii ubaguzi bali mshikamano-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres anmesema ana matumaini makubwa na vijana kwa sababu leo hii ukiangalia katika jamii kuna mwenendo wa tu kujificha kwao wenyewe, mwenendo wa watu kuwa na utaifa zaidi na kutokuwa wazi na mahitaji ya kuelewa kwamba changamoto za kimataifa zinahitaji suluhu ya kimataifa , ushirikiano wa kimataifa na taasisi za kimataifa.

Akizungumza kwenye chuo kikuu cha Cairo nchini Misri amesema kinyume chake , kwa kawaida vijana wanachangamana zaidi, ni wa kimataifa zaidi na walio wazi zaidi.

(GUTERRES CUT)

Hatuoni dhamira miongoni mwa vijana ya chuki dhidi ya wageni , au kutovumilia, au ubaguzi wa rangi, ambao kwa bahati mbaya sasa umeshamiri katika jamii zentu nyingi.Tunaona vijana wachukua hatua dhidi ya hili kwa aina mpya za mwingiliano na mshikamano na ndio sababu ninatumaini kwamba vizazi mpya vitakuwa na uwezo wa kufanya kile ambacho kizazi cha sasa haijaweza kufanya, ili kuimarisha demokrasia ya kimataifa utaratibu utawala ili kuruhusu amani kutawala katika dunia yetu.”

Guterres ameongeza kuwa anaamini tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana leo sio tuu ni tatizo baya kabisa kwa vijana ambao wanajiona hawana matumaini ya baadaye, sio tu pengo kubwa katika uwiano wa maendeleo kwa nchi, lakini pia limekuwa moja ya tisho kubwa kabisa la amani na usalama wa kimataifa.

(GUTERRES SAUTI )

“Hakuna kitu kibaya kama vijana wa kike na wakiume waliohitimu shahada za chuo kikuu kukosa ajira , kutokuwa na matumaini na kutokuwa na matarajio ya mustakhbali wao, na hakuna kitu rahisi kama taharuki hiyo na hasira zao kutumiwa na propaganda za mashirika ya itikadi kali kwa namna nyingine. Inaweza kuwa Da’esh lakini inaweza kuwa chama maarufu cha chuki dhidi ya wageni katika sehemu Fulani duniani, au tumeshuhudia hivi karibuni katika moja ya nchi mauaji ya kutisha yakitekelezwa na wanaopigania haki za weupe. Hivyo tunashuhudia itikadi kali katika mifumo tofauti , katika jia tofauti.”

Katibu Mkuu ameongeza kuwa taharuki inayotanda miongoni mwa vijana ambao hawana matumaini ya mustakhbali wao ni chanzo kikubwa cha kutokuwepo na usalama katika dunia ya sasa.