Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusipochukua hatua sasa ajenda ya kutokomeza njaa 2030 itakuwa ndoto:FAO

Tusipochukua hatua sasa ajenda ya kutokomeza njaa 2030 itakuwa ndoto:FAO

Kushindwa kuchukua hatua sasa kuhakikisha mifumo ya chakula inakuwa imara sanjari na mabadiliko ya tabia nchi, kutaleta zahma kubwa , katika uzalishaji wa chakula katika kanda nyingi na kuzamisha juhudi za kimataifa za kutokomeza njaa na umasikini ifikapo mwaka 2030.

Onyo hilo limetolewa Jumatatu na mkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo José Graziano da Silva ambaye amesisitiza kuwa kilimo kinashikilia ufunguo wa kutatua matatizo mawili makubwa yanayoukabili ulimwengu kwa sasa, utokomezaji wa njaa na kuchangia katika udhibiti wa mabadiliko ya tabia nchi. Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kimataifa wa serikali kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaofanyika mjini Dubai.

Da Silva amewataka washiriki kusaidia wakulima wadogowadogo katika nchi zinazoendelea ili wakabiliane na mabadiliko ya tabia nchi. Amesemaasilimia kubwa ya watu walio masikini kabisa na wanaokabiliwa na njaa duniani hutegemea kilimo.