Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio ni wewe! Tuitumie kuimarisha mashauriano-UNESCO

Radio ni wewe! Tuitumie kuimarisha mashauriano-UNESCO

Leo ni siku ya radio duniani ujumbe ukiwa Radio ni wewe ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limetaka chombo hicho kitumiwe kuchagiza mashauriano. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Tunaishi katika mapinduzi ambamo kwayo tunabadilishana na kupata taarifa na bado katika mabadiliko haya, Radio imesalia kuwa muhimu na shirikishi, ndiyo alivyoanza ujumbe wake mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova akitaka sasa mapinduzi hayo yachagize maendeleo endelevu.

Nchini Tanzania, kuu wa ofisi ya UNESCO, Zulmira Rodriguez akasema pamoja na mapinduzi hayo sasa ni vyema kuhakikisha kuwa..

(Sauti ya Zulmira)

“Tunawezaje kuwa na umuhimu kwenye jamii tunayohudumia badala ya kutumia radio kwa ajili ya maslahi mengine.”

Naye Waziri mwenye dhamana ya Habari nchini humo Nape Nnauye akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya radio duniani jijini Dar es salaam amesema..

(sauti ya Nape)