Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iran yagubika mkutano kuhusu udhibiti wa kuenea silaha

Iran yagubika mkutano kuhusu udhibiti wa kuenea silaha

Hii leo huko Geneva, Uswisi kumefanyika mkutano wa kudhibiti kuenea kwa silaha ambapo suala la Iran kufanya jaribio la silaha tarehe 29 mwezi uliopita liligubika kikao hicho.

Mathalani mwakilishi wa Marekani amesema jaribio hilo ni kinyume na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 2231, akisema kuwa kombora lililojaribiwa lina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.

Hata hivyo Iran imesema imeazimia kuwajibika na udhibiti wa silaha hizo ikitaja taarifa za hivi karibu za shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA kuwa ni shuhuda wa azma yake.

Imesema haina mpango wa kusaka silaha za nyuklia na wala haiamini kuwa silaha za nyuklia zitaiwezesha kuwa salama.