Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yazindua mwongozo wa kukabili saratani

WHO yazindua mwongozo wa kukabili saratani

Leo ni siku ya saratani duniani ambapo shirika la afya duniani, WHO linazindua mwongozo mpya wa kuwezesha uchunguzi wa mapema wa ugonjwa huo hatari unaosababisha vifo vya watu milioni 8.8 kila mwaka duniani, kati ya wagonjwa milioni 14 wanaobainikana ugonjwa huo.

WHO inasema hali si shwari kwani idadi inaongezeka mwaka hadi mwaka na hivyo njia pekee ni kuimarisha mbinu za kubaini mapema kwani hata visababishi vya saratani navyo vinaongezeka.

Shirika hilo linasema saratani haipaswi kusalia adhabu ya kifo wakati huu ambapo kuna kampeni za kudhibiti visababishi kama vile matumizi ya tumbaku, unywaji wa pombe na mlo usio bora.

Ili kufahamu mwongozo huo mpya unaozinduliwa leo unahusisha nini, Assumpta Massoi wa idhaa hii amezungumza na Dokta Alphoncina Nanai ambaye ni afisa anayehusika na magonjwa yasiyopatiwa kipaumbele, NTDs. Kwanza anaanza kwa kuelezea hatua zinazotajwa kwenye mwongozo huo.

image
Elimu kwa wanafunzi kuhusu saratani. (Picha:UNifeed Video)