Skip to main content

Nuru ya elimu hatimaye kung'aa Sudan Kusini

Nuru ya elimu hatimaye kung'aa Sudan Kusini

Nchini Sudan Kusini shule 60 zimehamishwa kutoka maeneo yenye mapigano ya Yei na kupelekwa katika eneo salama ndani ya mji kabla ya muhula mpya wa shule kuanza Februari 6. Taarifa zaidi na Rosemay Musumba.

(Taarifa ya Rose)

Kwa mujibu wa Radio ya Miraya ya Umoja wa Mataifa nchini humo, shule 45 za msingi zimechanganywa kwenye vituo vitatu na za sekondari 15 zimehamishiwa maeneo matatu ndani ya mji huo wa Yei.

Shule kadhaa nje kidogo ya mto Yei zilitelekezwa na hazikuwa salama kwa muda kutokana na mapigano, na mpango huu umekaribishwa vizuri na wazazi na wanafunzi

Mkurugenzi mkuu wa elimu ametoa wito kwa serikali na wadau wengine kutoa msaada wa lishe na vifaa vya shule kwa wanafunzi kabla ya shule kuanza..