Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM/UNHCR waiomba Marekani kuendeleza utu kwa wakimbizi na wahamiaji:

IOM/UNHCR waiomba Marekani kuendeleza utu kwa wakimbizi na wahamiaji:

Mahitaji ya wakimbizi na wahamiaji kote duniani hivi sasa ni makubwa kuliko wakati mwingie wowote, na mpango wa Marekani wa kuwapa makazi moja ya mipango muhimu sana duniani.

Kwa mujibu wa shirika nla Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM sera ya muda mrefu ya Marekani ya kuwakaribisha wakimbizi imekuwa hali ya ushindi kwa wote.

Kwani imeokoa maisha ya watu walioa na mahitaji zaidi duniani ambao wamelipa fadhila kwa kukumbatia na kuimarisha jamii zao mpya kwani mchango wa wakimbizi na wahamiaji katika mkazi yao mapya kote duniani umekuwa mzuri na wa faida.

IOM na UNHCR sasa wanatuami kwamba serikali ya Marekani itaendelea na jukumu la uongozi wake imara na utamaduni wa muda mrefu wa kuwalinda wale wanaokimbia vita na mauaji.

Mashirika hayo pia yamesema yataendelea kufanya kazi na uongozi wa Marekani katika lengo la pamoja la kuhakikisha usalama na makazi bora na miapango ya uhamiaji.

Pia mashirika hayo yamesema yanaamini kuwa wakimbizi wanastahili kutendewa sawa katika kupata ulinzi, msaada na fursa za kupewa makazi bila kujali dini, utaifa au rangi.