Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto bado wanakumbana na ukatili duniani: Gilmore

Watoto bado wanakumbana na ukatili duniani: Gilmore

Kamati ya haki za mtoto inayoangazia uetekelezaji wa mkataba wa haki za mtoto CRC imefungua kikao chake cha 74 mjini Geneva, ambapo imeelezwa kuwa hatua zimepigwa katika utekelezaji wa mkataba huo. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Wakati wa ufunguzi wa kikao hicho Naibu Kamishina wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Bi Kate Gilmore amesema mwaka 2016 kamati imefanikiwa kukamilisha ripoti na kupitishwa kwa mijadala ya wazi kuhusu utambuzi wa haki za watoto.

(Sauti Gilmore)

‘‘Hii inadhihirisha katika uhalisia namna watoto wanavyoweza kujumishwa katika michakato ya uamuzi na kuwa sehemu ya hatua dhidi ya mazingira ambayo yaweza kuwadhuru.’’

Amesema juhudi zaidi zahitajika kwani ukatili wa haki za mtoto bado unasalia.

( Sauti ya Gilmore)

‘‘Umasikini kwa watoto, ukatili wa kila aina na ubaguzi dhidi ya mtoto wa kike, watoto wanaozaliwa nje ya ndoa, watoto wenye ulemavu, wahamiaji na wasaka hifadhi, wasio na utaifa na wakimbizi. Kuendelea kwa haya kunadhihirisha kukosekana kwa ushirikiano wa mbinu sahihi za haki za watoto katika mipango na utekelezaji wa sera za ustawi wa mtoto na mipango.’’