Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia kukutana kwa ajili ya takwimu na maendeleo Afrika Kusini

Dunia kukutana kwa ajili ya takwimu na maendeleo Afrika Kusini

Mkutano wa kwanza wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa kuhusu takwimu, unatarajiwa kufanyika mjini Cape Town nchini Afrika Kusini ikiwa ni juhudi za kusongesha ajenda 2030 ya maendeleo endelevu.

Mkutano huo wa siku nne, kuanzia Januari 15 hadi 18 unaoratibiwa kwa pamoja kati ya ofisi ya takwimu ya Umoja wa Mataifa na kitengo cha takwimu cha idara ya uchumi na masuala ya kijamii, umeelezwa kuwa utawezesha kupatikana kwa usanifu wa takwimu kwa ajili ya maendeleo kimataifa.

Mkurugenzi wa kitengo cha takwimu cha uchumi na masuala ya kijamii katika Umoja wa Mataifa Stefan Schweinfest, amewaambia waandishi wa habari mjini New York leo kuwa mkutano huu umekuja wakati muafaka kwakuwa.

( Sauti Stefan)

‘‘Tunahitaji kupata takwimu ili tuelewe nini kinaendelea katika jamii kule wanakoishi. Pia kuweza kuziwajibisha tabaka mbalimbali za serikali kadhaa .’’

Kwa mara kwanza mkutano huu utawajumuisha wakufunzi kutoka asasi za kiraia ambao watashirikisha uzoefu na uelewa wao kuhusu umuhimu wa takwimu katika maendeleo.