Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vitokanavyo na tumbaku duniani kuongezeka ifikapo mwaka 2030

Vifo vitokanavyo na tumbaku duniani kuongezeka ifikapo mwaka 2030

Shirika la afya duniani, WHO limesema idadi ya watu wanaofariki dunia kila mwaka kutokana na matumizi ya tumbaku itafikia milioni Nane mwaka 2030 iwapo hatua hazitachukuliwa.

WHO imesema waaathirika zaidi ni nchi zinazoendelea au za kipato cha chini ambako nguvu ya soko la tumbaku imeshika kasi licha ya kampeni zinazoendelea kukabili matumizi ya bidhaa hizo.

Katika ripoti yake ya leo kuhusu mwenendo wa kiuchumi wa tumbaku na udhibiti wa bidhaa hiyo, WHO imesema ongezeko hilo la vifo ni moja ya mambo tisa ambayo yametokana na utafiti uliofanywa kwa ushirikiano na Marekani.

Jambo jingine linachochea idadi kuongezeka ni bidhaa za tumbaku kutoweka bayana maonyo ya athari za kiafya pamoja na nguvu kubwa ya kampuni za tumbaku katika nchi.

WHO imesema utafiti huo umebaini kuwa harakati za kudhibiti tumbaku hazina madhara kiuchumi na badala yake zinapunguza mzigo ambao maskini anaupata kwa kutumia tumbaku.

Halikadhalika umebaini harakati mbali mbali duniani za kudhibiti matumizi ya tumbaku lakini WHO imetaka juhudi za pamoja sambamba na uendelevu wa harakati hizo.